1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya kuweka chini silaha

19 Januari 2015

Wanamgambo wa kishia wameendeleza mapigano makali dhidi ya jeshi katika mji mkuu wa Yemen Sanaa katika kile kinachoangaliwa kama mtihani mkubwa kwa utawala wa rais Abdrabuh Mansur Hadi.

https://p.dw.com/p/1EMpS
Mapigano SanaaPicha: Reuters/K. Abdullah

Wanamgambo wa kishia wameendeleza mapigano makali dhidi ya jeshi katika mji mkuu wa Yemen Sanaa na magari yaliyoandamana na lile la waziri mkuu yameshambuliwa katika kile kinachoangaliwa kama mtihani mkubwa kwa utawala wa rais Abdrabuh Mansur Hadi.

Njama ya mapinduzi imetokea pale kundi la watu waliokuwa na silaha walipolihujumu kasri la rais mjini Sanaa-mji mkuu wa Yemen uliogubikwa na mapigano makali kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu mwezi wa septemba mwaka jana.Milio ya risasi imehanikiza na moshi kutanda katika mji mkuu wa Yemen Sanaa.

Wanamgambo wanaojulikana kama Huthi,wanadhibiti hivi sasa vyombo vya habari vya taifa na kuzidi kujiimarisha katika mji huo mkuu .Wanamgambo wa huthi wamekiteka pia kituo cha kijeshi kilichoko mlimani karibu na kasri la rais.

Watu wasiopungua watano wameuwawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mapigano karibu na kasri la rais na katika maeneo mengine ya mji mku-hayo ni kwa mujibu wa duru za hospitali.

Waziri mkuu Khalid Bahah amenusurika chupu chupu pale wanamgambo wa Huthi walipofyetulia risasi mlolongo wa magari yaliyoandamana na gari yake walipotoka katika kasri la rais Abdrabuh Mansur Hadi.Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa habari Nadia Sakkaf.

Huthi wanadai madaraka makubwa zaidi

Waziri mkuu Bahah alikuwa na mazungumzo pamoja na rais na mwakilishi wa wanamgambo wa Huthi katika juhudi za kufikia makubaliano ya kuweka chini silaha,magari hayo yalipofyetuliwa risasi.Na lile la mwakilishi wa wanamgambo wa Huthi pia limehujumiwa waziri wa habari Nadia Sakkaf amesema.

Kämpfe in Sanaa 19.01.2015 die Bevölkerung ergreift die Flucht
Watu wanayapa isogo maskani yaoPicha: Reuters/K. Abdullah

Wakaazi wa Sanaa hawajui chanzo halisi cha mapigano hayo mepya.

"Nilikuwa njiani kwenda kazini leo asubuhi katika mtaa wa Hadda,nilipowaona watu waliobeba silaha wameenea kila pembe.

Wakiangaliwa kama washirika wa Iran katika mapaigano ya kuania ushawishi dhidi ya Saud Arabia,wanamgambo wa Huthi wanaowakilishwa katika serikali ya mjini Sanaa hivi sasa,wanasema "hali haitotulia" ikiwa madai yao ya kugawana sawa madaraka na kutungwa katiba mpya hayatotekelezwa.Wahuthi wanadai haki zaidi kwa jamii ya Zaydi ya kishia nchini humo na wanaendesha kampeni dhidi ya rushwa.

Wito wa kusitisha mapigano

Mswaada wa katiba,ulioanzishwa jumamosi iliyopita umelenga kutatua matatizo ya kimkoa lakini wahuthi wanahofia katiba hiyo isije ikawapunguzia madaraka.

Kämpfe in Sanaa 19.01.2015
Mapigano SanaaPicha: Reuters/K. Abdullah

Wakati huo huo jumuia ya nchi za kiarabu imezisihi pande zote zinazohusika zisitishe mapigano nchini Yemen na kuheshimu viongozi halali wa nchi hiyo.

Mwadishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/AP/Reuters/

Mhariri:Josephat Charo