1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
HistoriaAfrika

Njoya Ibrahim: Mfalme wa kisasa wa Kamerun

Yusra Buwayhid
26 Februari 2021

Ingawa Mfalme Njoya Ibrahim alitawala wakati wakoloni wa Kijerumani walipoingia Cameroon, aliweza kuongoza watu wake kwa uhuru. Mfalme huyo wa Bamum alijulikana kama mvumbuzi na mwenye huruma kwa watu wake.

https://p.dw.com/p/3pxeH

Njoya Ibrahim: Mfalme wa kisasa wa Kamerun

Njoya Ibrahim alizaliwa mwaka gani?

Njoya Ibrahim alizaliwa mwaka 1876 katika eneo linalojulikana sasa kama Cameroon. Na alikuwa wa miaka mitatu tu baba yake Nsangou alipofariki vitani. Kutoka mwaka 1879 hadi 1887, mama yake, Na Njapdnunke , alimkamatia utawala kwa muda akisaidiwa na Gbetnkom Ndombu. Alikaa kwenye kiti cha enzi akiwa na umri mdogo wa miaka 11, na kuwa mfalme wa 17 wa nasaba ya Ncharé Yen. Alitawala kwa miaka 46 hadi Mei 30, 1933, alipofariki akiwa uhamishoni mjini Yaoundé.

African Roots | Sultan Njoya Ibrahim
Asili ya Afrika | Mfalme Njoya Ibrahim

Njoya Ibrahim alikuwa mfalme wa aina gani?

Tofauti na waliomtangulia, Mfalme wa Bamum hakuwa katili. Alilazimishwa kwenda vitani akiwa na umri mdogo. Mwaka 1892, alimfukuza mfanyakazi wake Gbetnkom Ndombu - ambaye alikuwa na uchu wa madaraka - na hata kujaribu kuanzisha kikosi cha uasi cha kumuondoa madarakani mfalme huyo mpya. Kutokana na hayo, kulizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitatu hadi mwaka 1895, wakati mfalme Njoya aliposhinda vita hivyo. Alisaidiwa na mfalme Fula wa Banyo, sultan Oumarau, anaetokea kaskazini mwa Cameroon.

Ni nini kilichoufanya Ufalme wake kuwa na nguvu?

Njoya Ibrahim alikuwa kiongozi mwenye haiba na asiyependa vita lakini pia alikuwa mvumbuzi mkubwa. Mnamo mwaka 1915, aliunda dini iliyochanganya mafundisho ya dini ya Kiislam na Kikiristo. Mafundisho ya dini hiyo yaliandikwa kwenye kitabu kilichoitwa Nkuet Kwate au Biblia ya Mfalme. Na kiliandikwa kwa lugha ya A-Ka-U-ku, iliyovumbuliwa na mfalme Njoya mwenyewe na inayotokana na lugha ya shümom. Mfalme Njoya pia aliandika vitabu vingine kumi na tano (ikiwa ni pamoja na riwaya za mapenzi) na ensaiklopidia kuhusu dawa za kitamaduni.

Halikadhalika, alivumbua mashine ya kusagia mahindi. Na aliendeleza utamaduni na sanaa wa watu wa Bamum. Mji mkuu wa Foumban unajulikana kama mji wa sanaa hii leo. Kasri alilolijenga Njoya Ibrahim mjini humo, linalindwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.

African Roots | Sultan Njoya Ibrahim
Asili ya Afrika | MfalmeNjoya Ibrahim

Alikuwa na uhusiano gani na wakoloni?

Tofauti na Rudolf Duala Manga Bell, Njoya Ibrahim hakupigana na wakoloni. Mwaka 1906 kwa mfano, alishirikiana na Wajerumani katika vita vyake dhidi ya Banso aliyemuua baba yake na kuzuia fuvu lake kama ushahidi wa kumuua mfalme huyo. Ushirikiano huo ulikuwa ndiyo mwanzo wa uhusiano mzuri kati ya wakoloni wa Ujerumani na watu wa Bamum. Mnamo mwaka 1908, Njoya Ibrahim alitumtumia mfalme William II kiti chake cha enzi kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa. Leo hii, kiti hicho cha enzi kinaonyeshwa katika makumbusho ya Ethnolojia mjini Berlin. Pia alimtunukia Jesko von Puttkamer -  aliyekuwa akitawala Kamerun wakati huo - mmoja wa wake zake bado akiwa bikira, na kumzalia mtoto anaitwa Elise.

Ingawa uhusiano kati ya Ujerumani na watu wa Bamuns kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni mzuri, hali hiyo ilibadilika pale walipowasili wakoloni wa Ufaransa mwishoni wa Vita vya Pili vya Dunia. Wakoloni wa Kifaransa waliusimamisha utawala wake na kumsafirisha hadi Yaoundé (kwa sababu bado hadi leo hazijafafanuliwa). Alifariki dunia akiw ana huzuni kubwa  Mei 30, 1933, baada ya kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa miaka mitatu.

African Roots | Sultan Njoya Ibrahim
Asili ya Afrika | Mfalme Njoya Ibrahim

Ni misemo gani maarufu ya mfalme Njoya?

"Bora kufa kuliko kuaibika." Ndiyo maana alihiari kufa Yaounde kuliko kuabishwa mbele za watu wake wa Bamum na kukamatwa kama mfungwa.

"Iwapo mtu atakuzidi nguvu, jifunze kubeba begi lako na kutembea nyuma yake." Msemo wake huu ndiyo unaoakisi uamuzi wake wa kuwakaribisha vizuri walowezi wa kwanza Wajerumani katika ufalme wake.

"Usiruhu watu kukuchukulia maamuzi." Kulingana na Oumarou Nsangou, mwalimu wa lugha ya shü-mom, nukuu hii inaunga mkono msemo wa mwanafalsafa Immanuel Kant ambaye alisisitiza kila mtu kuwa na "uthubutu wa kufikiria mwenyewe."

Njoya Ibrahim: Mfalme wa kisasa wa Kamerun

Ushauri wa kisayansi kuhusu makala hii umetolewa na wanahistoria Profesa Doulaye Konaté, Lily Mafela, Ph.D., na Profesa Christopher Ogbogbo. Mfululizo wa makala za Asili ya Afrika umefadhiliwa na Taasisi ya Gerda Henkel.