1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nokia yachunguzwa kukiuka kanuni za ruzuku

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyP0

BOCHUM: Kwa mujibu wa gazeti la Kijerumani la kila juma Focus,waendesha mashtaka wa serikali wanaichunguza kampuni kubwa ya Kifini-Nokia kuhusu madai kwamba kampuni hiyo imekwenda kinyume na kanuni za ruzuku.Msemaji wa Wizara ya Uchumi ya mkoa wa North Rhine-Westphalia amesema,kati ya mwaka 2002 na 2005 kampuni ya Nokia iliajiri watu 400 wachache kuliko vile ilivyokubaliwa.

Nokia ina mpango wa kufunga kiwanda chake katika mji wa Bochum mkoani North Rhine-Westphalia na kwa sehemu kubwa kuhamisha kazi zake nchini Rumania. Hatua hiyo humaanisha kuwa watu 2,300 watakosa ajira.Hii leo wafanyakazi hao wamekutana Bochum kushauriana njia ya kugombea nafasi zao za kazi.