1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOUACKCHOTT: Steinmeier amemaliza ziara ya nchi za Maghreb

19 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrO

Waziri wa masuala ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amekamilisha ziara yake ya juma moja katika nchi za Maghreb barani Afrika kwa kuitembelea Mauritania.Steinmeier alikutana na rais wa Mauritania Ely Ould Mohamed mjini Nouakchott.Baada ya serikali kubadilishwa mara nyingi nchini humo,leo hii kwa mara ya kwanza kunafanywa chaguzi za bunge na mabaraza ya mitaa.Ujerumani na Umoja wa Ulaya zimesaidia kutayarisha chaguzi hizo na wajumbe wake wanasimamia utaratibu wa uchaguzi.Ziara ya Steinmeier ni ya kwanza kupata kufanywa na waziri wa kigeni wa Ujerumani nchini Mauritania tangu miaka 35.