1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOUAKCHOTT: Uchaguzi wa bunge na madiwani kufanyika jana nchini Mauritania

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr4

Raia nchini Mauritania walipiga kura jana kwenye uchaguzi wa kwanza wa bunge na madiwani ikiwa ni mwaka moja baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliomtoa madarakani rais Maaouiya Ould Sid Ahmed Taya. Wachunguzi wa kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya kiarabu, Arab League, wamesema watu wengi wamejitokeza kupiga kura na kwamba hakuna matatizo yaliotokea. Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutolewa hii leo. Hata hivyo, uchaguzi wa bunge utaendelea mwezi ujao. Uchaguzi wa rais na baraza la seneti umepangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao.