1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nouakchott. Wagombea wawili kukutana katika duru ya pili ya uchaguzi March 25.

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJk

Wagombea wawili katika uchaguzi mkuu wa rais nchini Mauritania watakutana tena katika duru ya pili ya uchaguzi hapo March 25, wizara ya mambo ya ndani imesema jana kwa msingi wa matokeo kamili baada ya uchaguzi wa siku ya Jumapili .

Waziri wa zamani Sidi Ould Cheikh Abdallahi amepata asilimia 24.79 ya kura , akimtangulia mwanasiasa maarufu wa upinzani Ahmed Ould Daddah , ambaye amepata asilimia 20.68 ya kura kwa mujibu wa maafisa.

Wagombea wawili wa mwanzo wote wamemaliza duru ya kwanza vizuri lakini chini ya asilimia 50 zinazohitajika kwa ajili ya kupata ushindi wa moja kwa moja katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia katika nchi hiyo iliyoko kaskazini magharibi ya bara la Afrika. Wapiga kura wamepiga kura zao wakitaraji kumaliza miaka kadha ya tawala za kijeshi na udikteta.