1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOVOKUZNETSK:Mazishi yaanza Urusi baada ya mikasa wiki hii

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGl

Mazishi ya mwanzo kufuatia mikasa miwili nchi Urusi yanaendelea baada ya mlipuko wa mgodi mjini Siberia vilevile kuteketea kwa nyumba ya wazee na kudondoka kwa ndege mjini Samara.

Waombolezaji waliobeba mashada ya maua walitazama majeneza ya maiti hizo katika kanisa la Spaso-Preobrazhensky.

Mazishi ya wazee waliopoteza maisha yao wakati nyumba yao ilipoteketea yanafanyika hapo kesho.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza leo kuwa siku ya kitaifa ya maombolezi kufuatia vifo vya watu 200 katika juma hili pekee katika mikasa tofauti.

Mgodi mmoja umelipuka siku ya Jumatatu katika eneo la Siberia na kusababisha vifo vya takriban watu 106 huku moto ukiteketeza nyumba moja ya wazee kwenye eneo la Krasnodar kusini mwa Urusi na kusababisha vifo vya watu 63 mpaka sasa.Watu 7 walifariki dunia siku ya jumamosi na wengine 50 kujeruhiwa pale ndege moja ya abiria ilipodondoka mjini Samara katikati ya Urusi