1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nuremberg: Ukosefu wa kazi Ujerumani umepungua katika mwezi huu wa Februari

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNr

Ukosefu wa kazi hapa Ujerumani umepungua na kufikia asilimia 10.1 katika mwezi huu wa Februari kutoka asilimia 10.2 mwezi uliopita. Idadi ya Wajerumani wasiokuwa na kazi imepungua na kufikia milioni 4.22, ukilinganisha na milioni 4.24 mwezi uliopita. Hali hiyo imesababishwa kwa vile majira ya baridi hayajawa makali mara hii na bidhaa nyingi zimesafirishwa ngambo.