1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nuri al Maliki asema ratiba ya kuondoka majeshi ya Marekani iwekwe

Saumu Mwasimba8 Julai 2008

Je pendekezo hilo la Iraq linakubaliwa na rais Bush?

https://p.dw.com/p/EY38
Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-MalikiPicha: AP

Kwa mara ya kwanza waziri mkuu wa Iraq Nouri al Maliki ametamka wazi hadharani kwamba nchi yake inataka paweko ratiba ya kuondoka nchini Iraq wanajeshi wa Marekani pamoja na suala hilo kujumuishwa katika mazungumzo yanayoendelea na serikali ya mjini Washington.

Waziri mkuu huyo wa Iraq hakutoa maelezo zaidi juu ya suala hilo lakini mshauri wa masuala ya kiusalama wa taifa amefahamisha kuwa serikali imeandaa mapendekezo ya kutaka itolewe ratiba ya wanajeshi hao wa Marekani kuondoka Iraq itakayotokana na uwezo wa vikosi vya Iraq wa kuweka hali ya usalama nchini humo.

Hata hivyo mjini Washington wizara ya mambo ya nje imekataa kutoa tamko lolote kuhusiana na kuendelea mazungumzo kama hayo na Iraq.

Rais Goerge W Bush anapinga vikali pendekezo hilo.