1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nuri al Maliki ataka jeshi la Marekani liwe Irak hadi 2008

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTXd

Waziri mku wa Irak, Nuri al Maliki, anasema mwaka ujao wa 2008 utakuwa mwaka wa mwisho kwa majeshi ya Marekani yanayohudumu nchini Irak chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa. Baadaye, nafasi ya tume hiyo itachukuliwa na mkataba mpya wa usalama utakaosainiwa kati ya Irak na Marekani.

Nuri al Maliki na rais George W Bush wamekubaliana juu ya tangazo la kanuni zitakazoyaongoza mazungumzo ya kuunda uhusiano wa muda mrefu kati ya Irak na Marekani.

Msingi wa kanuni hizo ni kuilinda demokrasia nchini Irak dhidi ya vitisho kutoka nje.

Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imesema mazungumzo yataanza mapema mwaka ujao na yanatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai.