1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NYALA: Rais wa Sudan atoa wito wa kuwa na amani

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgV

Rais wa Sudan Omar al-Bashir ametoa wito wa kuwa na amani.Alitamka hayo,wakati wa ziara ya nadra katika jimbo la mgogoro la Darfur. Alipozungumza mjini Nyala kusini mwa Darfur,Rais el-Beshir alitoa wito kwa waasi ambao hawakutia saini makubaliano ya amani ya mwezi Mei mwaka 2006,waungane na mchakato wa kisiasa ili waweza kushirikiana katika ukarabati wa jimbo la Darfur lililokumbwa na vita.

Serikali ya Sudan imekubali mpango wa kupeleka Darfur,vikosi vya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.Vikosi hivyo vitashirikiana kulinda amani katika jimbo hilo la mgogoro na vitachukua nafasi ya majeshi ya Umoja wa Afrika yaliyokuwepo huko hivi sasa yakiwa na upungufu wa pesa na zana.