1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyota wa Ghana wapepea bendera ya Afrika

P.Martin/DPA/RTRE24 Juni 2010

Ujerumani imesonga mbele katika duru ya pili ya michuano ya kuwania Kombe la Dunia inayoendelea nchini Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/O1Pg
Germany's Bastian Schweinsteiger, left, Germany's Lukas Podolski, center, and Ghana's Kwadwo Asamoah fight for the ball during the World Cup group D soccer match between Ghana and Germany at Soccer City in Johannesburg, South Africa, Wednesday, June 23, 2010. (AP Photo/Gero Breloer)
Bastian Schweinsteiger(kushoto) na Lukas Podolski(kulia) wa Ujerumani, wakikwaruzana na Kwadao Asamoah wa Ghana (kulia) katika mchuano wa Kombe la Dunia uwanjani Soccer City, Johannesburg, 23 Juni,2010.Picha: AP

Hiyo jana, Ujerumani ilinusurika, baada ya kuilaza Ghana kwa bao 1-0 katika mchezo wa kufa kupona, pande hizo mbili zilipokumbana uwanjani Soccer City mjini Johannesburg.

Baada ya kuchuana kwa dakika sitini nzima, Mesut Oezil wa Ujerumani, aliuvurumisha mpira katika wavu wa Ghana na hivyo kuinusuru Ujerumani kufunga virago na kurejea nyumbani katika duru ya mwanzo ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa.

Hata hivyo, Ghana iliitoa jasho Ujerumani na imethibitisha kuwa wao kweli ni nyota. Ghana ni timu pekee kutoka Afrika kubaki katika kundi la timu 16 za mwisho, katika kinyanganyiro hicho cha Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini. Nyota hao wa Ghana, watakumbana na Marekani jumamosi ijayo. Hiyo jana Marekani iliifunga Algeria bao 1-0 na Australia nayo iliicharaza Serbia mabao 2-1.Uingereza pia hiiyo jana ilinusurika kufunga virago, baada ya kuikandika Slovenia bao 1-0.

England's Wayne Rooney controls the ball between Slovenia's Aleksander Radosavljevic, left, and Slovenia's Miso Brecko, right, during the World Cup group C soccer match between Slovenia and England at Nelson Mandela Bay Stadium in Port Elizabeth, South Africa, Wednesday, June 23, 2010. (AP Photo/Roberto Candia)
Wayne Rooney wa Uingereza(katikati) akikumbana na Aleksander Radosavljevic na Miso Brecko(kulia) wa Slovenia katika mchuano wa Kombe la Dunia, 23 Juni 2010.Picha: AP

Uingereza itateremka tena uwanjani siku ya Jumapili kwa mchezo unaongojewa kwa hamu kubwa. Siku hiyo, Uingereza itakwaruzana na Ujerumani.