1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyumba ya wagonjwa wa watumiaji madawa

17 Februari 2017

Kwa mtazamo wa wengi, Zanzibar inaonekana kuwa kama kisiwa cha peponi. Lakini katika raha za pepo hiyo, utumiaji wa madawa ya kulevya na usambazaji wake umekuwa ugojwa sugu kisiwani humo.

https://p.dw.com/p/2XlwP
Sansibar Stonetown Heroinsüchtige Sober House
Nyumba ya sober iliyopo mji mkongwe wa Unguja inatibu watumiaji heroinPicha: DW/M. Hartlep

Utumiaji wa madawa ya kulevye umekuwa ni ugojwa mkubwa unaoukabili kisiwa cha Zanzibar. Mbali na utumiaji wa madawa hayo, Zanzibar inatumiwa kama njia kuu ya kuuingiza madawa hayo Afrika na vigogo wa kimataifa biashara hiyo.

Serikali kwa sasa inajaribu sana kukabiliana na tatizo la madawa ya kulevya, kwa kuzuia uingiaji wa madawa kisiwani humu.

Hakimu alikuwa akimtazama mwenzake aliyekuwa amelala chini huku akikumbukia jinsi gani na yeye siku za  mwanzo, alivyokabiliana na mateso ya maumivu., alipoanza kuachana na madawa ya kulevya ya heroin.

Sansibar Stonetown Heroinsüchtige Sober House
Nyumba ya matibabu ya utumiaji madawa ya kulevyaPicha: DW/M. Hartlep

" Ilikuwa inauma sana, mwili ulikuwa na maumivu makali. Siku ya mwanzo nilikuwa kama huyu kijana aliyelala pale;" alisema Hakimu

Hakimu ana umri wa miaka 51, amedhoofika mpaka nguo zake zinaonekana kuwa ni kubwa sana kwake, miguu yake iimejaa makovu, yupo katika matibabu. Kila mmoja kati ya wagojnwa 20 waliokuwepo katika nyumba ya matibabu ya utumiaji wa madawa ya Spartan amepitia adhabu hiyo kali ya maumivu katika mikakati ya kuuchana na madawa ya kulevya ya heroin.

Ndani ya nyumba hiyo kuna bango lililochujuuka lililoamrisha watumiaji madawa wafuate hatua 12 za kuachana na madawa ya kulevya.

Bango jengine pia linasema " Siku baada ya siku" na "pole pole ndio mwendo."

Sansibar Stonetown Heroinsüchtige Sober House
bango lililopo katika nyumba ya sober ya Zanzibar lisemalo: siku baada ya sikuPicha: DW/M. Hartlep

Sehemu hii ambayo sio mbali na mji mkongwe wa Unguja iliyomo ndani ya kuta kubwa, na iliyozungukwa na mageti ya nyumba za tabaka la kati, hapo ndipo wale wazanzibari waliokata tamaa wanapokuja kutafuta msaada.

Utumiaji wa madawa Zanzibar ni ugonjwa ulioenea.  Tokea miaka ya 1980 kisiwa hiki kimekuwa ndio sehemu kubwa ya upitishaji wa madawa ya heroin kuto Afghanistan kuingilia Afrika kupitia bahari ya bara hindi.

Lakini tokea 2010 kumekuwa na mikakati ya kupigana na uingizaji wa madawa kisiwani Zanzibar. Takwimu zinaonenya kuwa kuanzia kilo 200 mpaka 400 zilikamatwa katika baadhi ya miaka, alisema David Dadge, msemaji wa umoja wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa ya kulevya.

Sansibar Stonetown Heroinsüchtige  Sober House
watumiaji madawa ya kulevya wanaotibiwa Sober House ZanzibarPicha: DW/M. Hartlep

Uingizaji wa madawa ya kulevya Zanzibar

Kwavile fukwe za Zanzibar huwa zimejitenga, kisiwa hiki hutumiwa sana katika upitishaji wa madawa ya kulevya. Ingawa madawa hayo mengi husafirishwa kuelekea njia za kusini kama inavoitwa, ikimaanisha Afrika ya kusini na ya kati, madawa hayo mengi pia humalizikia katika soko la Zanzibar .

 Jumah Abdul Zidikheiry afisa wa ngazi ya juu anayeongoza uchunguzi na vita vya kukabiliana na madawa ya kulevya, alikuwa na haya ya kusema:

 "Kukabiliana na madawa ya kulevya sio rahisi. Sio kama kukabiliana na malaria. Malaria utatafuta chandurua, au utapiga dawa na tatizo limekwisha. Utumiaji wa madawa unaathiri nchi, unaathiri kila kitu."

Zanzibar, inahitaji msaada kutoka nje kukabiliana na tatizo hili, labda kutoka Ulaya au Marekani. Kwa sababu swali hili la madawa linaathiri uchumi wa kisiwa hiki na kuvunja jamii, aliendela kusema Zidikheiry.

Mwandishi:  Najma Said

Muhariri     : Daniel Gakuba