1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama amshinda Clinton jimboni Wyoming

Charo, Josephat9 Machi 2008

Obama adhihirisha umaarufu wake licha ya kushindwa katika majimbo matatu Jumanne iliyopita

https://p.dw.com/p/DLGC
Barack Obama (kulia) na Hillary ClintonPicha: AP

Seneta Barack Obama wa jimbo la Illinois amemshinda mpinzani wake seneta Hillary Clinton wa jimbo la New York katika kinyang´anyiro cha kutafuta uteuzi wa chama cha Democratic kugombea urais wa Marekani.

Katika uchaguzi wa awali uliofanyika jana katika jimbo la Wyoming, Obama amemshinda Clinton hivyo kupunguza kasi ya ushindi wa mpinzani wake aliyeshinda chaguzi tatu kati ya nne zilizofanywa Jumanne wiki iliyopita.

Jimbo la Wyoming lenye idadi kubwa ya wafuasi wa chama cha Republican, lina wajumbe 12 pekee watakaoshiriki kupiga kura kumchagua mgombea urais wa chama cha Democratic katika mkutano mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.

Wakati huo huo, Barack Obama amefutilia mbali uwezekano wa yeye kugombea kuwa makamu wa rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic huku Clinton akigombea kama rais. Matamshi hayo ya Obama yanapingana na matamshi ya Clinton ya hivi majuzi alipopendekeza kuwa tayari kugombea urais wa Marekani huku Obama akiwa makamu wake.