1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama asema Hillary Clinton hawezi kushinda urais wa Marekani

31 Januari 2008
https://p.dw.com/p/D05e

Seneta Barack Obama amesema mpinzani wake wa chama cha Democratic, Hillary Clinton, hawezi kushinda urais wa Marekani.

Obama amemlaumu Clinton akisema atakigawa chama na kuungana na chama cha Republican katika maswala ya biashara, jukumu la watu wanaowashawishi wabunge katika siasa na usalama wa kitaifa. T

imu ya kampeni ya Hillary Clinton imesema Obama anakiuka ahadi yake ya kufanya kampeni isiyo na malumbano.

Wakati huo huo, mgombea urais wa chama cha Democratic, John Edwards, amejiondoa katika kinyang´anyiro hicho.

Edwards amesema hajui ni nani atakayeshinda lakini lakini ana hakika chama cha Democratic kitashinda urais.

Mgombea urais wa chama cha Republican, Rudy Giuliani, pia amejiondoa.