1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama ataka bunge liamue kuhusu Syria

1 Septemba 2013

Kwa muda wa zaidi ya wiki sasa , Ikulu ya Marekani ya White House imekuwa ikielekeza mashambulizi yake kuelekea kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria. Lakini hayo yamebadilika rais Obama anataka sasa bunge liamue.

https://p.dw.com/p/19Zex
GettyImages 178936505 WASHINGTON, DC - AUGUST 31: (AFP OUT) U.S. President Barack Obama (R) joined by Vice President Joe Biden delivers a statement on Syria in the Rose Garden of the White House on August 31, 2013 in Washington, DC. Obama states that he will seek Congressional authorization for the U.S. to take military action following the events in Syria. (Photo by Kristoffer Tripplaar-Pool/Getty Images)
Barack Obama akizungumzia kuhusu SyriaPicha: Kristoffer Tripplaar-Pool/Getty Images

Uamuzi wa Rais Barack Obama wa ghafla badala yake wa kuomba ruhusa ya bunge unamuweka katika hatari ambayo inaweza kuharibu hali yake ya kuaminika iwapo hakuna hatua itakayochukuliwa kujibu shambulio la silaha za kemikali ambalo limekiuka kile binafsi alichosema kuwa ni kuvuka "mstari mwekundu".

Bunge la Marekani halijatatua karibu chochote cha maana tangu mwaka 2010, likishindwa kukamilisha kile ambacho hapo kabla kilikuwa wajibu wa msingi kwa masuala ya barabara , shule , mashamba na masuala ya mawasiliano nchini Marekani.

US President Barack Obama (L) delivers the State of the Union address to a joint session of Congress on Capitol Hill in Washington DC, USA, 27 January 2010. The State of the Union address comes one year and one week after Obama took office. President Obama is speaking on a wide variety of issues such as the federal deficit, unemployment, health insurance reform, campaign contributions and foreign policy. EPA/MIKE THEILER
Baraza la Congress mjini WashingtonPicha: picture-alliance/dpa

Kuomba ruhusa ya baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican pamoja na baraza la seneti linalodhibitiwa na chama chake cha Democratic kukubali kuchukua hatua za kijeshi , suala ambalo tayari lina utata ndani na kati ya vyama hivyo , inaingiza hali nyingine ya kutokueleweka kuhusiana na jibu la Marekani katika mzozo wa Syria.

Uwezo wa rais

Mabadliko hayo ya ghafla pia yanazusha maswali juu ya uwezo wa rais wa maamuzi na inaweza kuwafanya viongozi wa Syria, Iran, Korea ya kaskazini na kwingineko , kuwa na kichwa kigumu , na kusababisha wapate hisia kuwa rais wa Marekani hayuko tayari kuchukua hatua pale anaposema anaweza kufanya hivyo.

Bunge la Marekani hata hivyo halitaanza vikao hadi Septemba 9, kwa hiyo alama ya kuuliza itaendelea kuwepo katika sera za Marekani kuhusu suala la Syria kwa muda wa wiki, huku kukiwa na hisia kali pamoja na huenda mijadala yenye mvutano.

Hakuna mtu ambaye analijua baraza hilo la Congress vizuri ambaye alikuwa tayari kutabiri kwa uhakika kile kinachoweza kutokea katika azimio la kuiruhusu nchi hiyo kuishambulia Syria. Hali hiyo ya kutokuwa na uhakika inazidishwa mara nyingi na uhusiano mbaya na wa mbali wa Obama na bunge la Marekani.

Ufaransa nayo yapata kigugumizi

Ikiakisi sera za Marekani ,Ufaransa nayo itasubiri bunge lake kuangalia uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria kabla ya rais Francois Hollande kuamua iwapo nchi hiyo iishambulie Syria ama la .

French President Francois Hollande arrives for the European Council meeting at the EU headquarters in Brussels on June 27, 2013. European Commission President Jose Manuel Barroso on Thursday announced a political deal on the EU's hotly contested 2014-2020 trillion-euro budget, hours before an EU summit mulls how to get millions of jobless youths back into the workplace. AFP PHOTO / GEORGES GOBET (Photo credit should read GEORGES GOBET/AFP/Getty Images)
Rais wa Ufaransa Francois HollandePicha: Getty Images

Ufaransa imefuata karibu njia moja na Marekani wakati ikisisitiza kuwa inachukua uamuzi huru baada ya rais Barack Obama kusema jana Jumamosi (31.08.2013) kuwa anaamini Marekani inapaswa kuchukua hatua za kijeshi kuhusiana na shambulizi la gesi ya sumu linalotuhumiwa kufanywa na utawala wa rais Bashar al-Assad, lakini badala yake akaamua kulipeleka suala hilo bungeni.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / rtre

Mhariri. Caro Robi