1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama aunga mkono ndoa za jinsia moja

10 Mei 2012

Rais wa Marekani, Barack Obama, ameunga mkono ndoa za jinsia moja, huku maamuzi hayo yakibadilisha msimamo wake wa awali.

https://p.dw.com/p/14sha
Vijana mashoga na wasagaji wa Marekani wakifutilia tamko la kuunga mkono ndoa za mashoga
Vijana mashoga na wasagaji wa Marekani wakifutilia tamko la kuunga mkono ndoa za mashogaPicha: dapd

"Nimefanya maamuzi ya kimapinduzi na lazima Wamerikani wote watendewe sawa.'' Alisema  Rais Obama  kwa upole katika sentensi yake ya Kwanza kutoka kinywani kwa Rais huyo wa Marekani wakati akifanya mahojiano na Televisheni ya ABC nchini  Marekani na kukubali ndoa hizo.

Mitt Rommney ampinga ushoga

Keki katika mojawapo ya ndoa
Keki katika moja ya ndoaPicha: dapd

Huku Mitt Rommney ambaye ni mgombea wa kutoka chama cha Republican, ambaye anaonekana kuwa mpinzani mkubwa wa Obama akiwa katika jimbo Oklahoma, amepinga wazi ndoa za jinsia moja na kusema wazi ndoa ni kati ya mwanamke na mwanamume.

Maamuzi haya ya Rais Obama ni ya kimapinduzi, yameungwa mkono na kupongezwa sana na Wamerekani wanaounga mkono ndoa hizo na kusema rais wao amefikia maamuzi hayo baada ya kutakiwa kuunga mkono ndoa hizo kwa muda mrefu.

Huku mmojawapo wa mashoga hao, Stuat Kopperman, akifurahishwa na maamuzi ya rais wake, amechangia dola 25 katika mfuko wa bajeti ya kampeni za Rais Obama ili aweze kurejea tena Ikulu kwa mara ya pili kumalizia kipindi chake cha mwisho.

Katika mahojiano hayo na televisheni, Rais Obama amesema anaunga mkono hilo si kwa mabinti zake Sasha na Malia bali analikubali hilo kutokana na mambo kadhaa.

"Nimekuwa makini, kuna watu wengi wanaamini kuwa ndoa ya mwanamume na mwanamke inasimamia misingi ya dini, lakini watu wengi, majirani, wasaidizi wangu,wanajeshi wanaolinda taifa hili wanashiriki ndoa za jinsia moja." Amenukuliwa Rais Obama katika mahojianao hayo na ABC.

Msimamo wa ushoga ndani ya vyama vya siasa

Katika utafiti uliofanywa nchini Marekani hivi punde, umebaini kuwa asilimia 50 ya Wamerikani wanaunga mkono ndoa za jinsia moja, huku asilimia 48 wanapinga  ndoa hizo. Ndani ya Chama cha Rais Barack Obama cha Demokratiki inaonekana wazi kuwa kati ya wanachama, wawili wa chama hichi wanaunga mkono ndoa za jinsia moja, lakini Mdemokratiki mmoja anapinga. 

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: dapd

Hali ni kinyume kwa chama cha Republican, kwani wao wengi wanapinga ndoa za jinsia moja kwa kiwango cha juu zaidi. Wakati chama cha Independent wanaounga mkono ndoa za njisia moja ni asilimia 57 na wanaopinga ni asimilia 40 tu.

Mwandishi:Adeladius Makwega/APE

Mhariri:  Miraji Othman