1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama barani Ulaya

Oumilkher Hamidou6 Aprili 2009

Jinsi rais mpya wa Marekani alivyowavutia viongozi wa ulaya na dunia

https://p.dw.com/p/HRB7
Barack Obama mjini PraguePicha: AP

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wamejishughulisha zaidi na ziara ya rais wa Marekani Barack Obama barani Ulaya,na kuteuliwa katibu mkuu mpya wa jumuia ya kujihami ya NATO.

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE linazungumzia mikutano ya kilele ya wiki iliyopita na kuchambua jinsi Barack Obama alivyojitokeza katika jukwaa la kimataifa.Gazeti linaendelea kuandika:

"Washiriki wa mkutano wa kilele wa G-20,washirika wa NATO na wakuu wa Umoja wa Ulaya wamejipatia fursa ya kumpima rais huyo mpya wa Marekani atakaekua na usemi pia katika mustaakbal wa nchi zao kwa miaka inayokuja.Machoni mwao Obama hajajitokeza kama ,"kiongozi mjuaji wa dunia",bali kama "mtu mpya" anaetaka kujifunza. Obama amejitokeza kama mpatanishi ambae katika masuala muhimu ya malumbano yuko tayari kupatanisha na kuhakikisha mada tete inafumbuliwa kabla ya kufikishwa katika meza ya mazungumzo.Hiyo ni aina ya uongozi unaothaminiwa sana na wazungu wa Ulaya.Lakini wakitaka kuwa wakweli basi wanabidi wakiri pia kwamba uongozi wa ridhaa una kikomo pia.Itafika siku tuu ambapo rais atalazimika kupitisha maamuzi yasiyo ya kuridhisha.


Hayo ni maoni ya FAZ-Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linajishughulisha na tangazo la Obama la "kuitakasa dunia na silaha za kinuklea."Gazeti linaendelea kuandika:

"Dhamiri za Barack Obama za kuitakasa dunia na silaha za kinuklea mtu anaweza kusema ni ndoto;hata hivyo dhamiri hiyo imepindukia ndoto baada ya kuendelea na vitisho bila ya matumaini ya kuwa salama.Mkakati unahitajika kwa hivyo.Obama ameshafungua mlango.Njia kuelekea dunia iliyotakaswa na silaha za kinuklea inabidi ichongwe kwa msaada wa siasa muruwa."


Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linahisi hata rais ana haki ya kuota.Gazeti linaendelea kuandika:

Pengine kuna wanaohisi hii ni ndoto tuu Barack Obama aliyoizungumzia mjini Prague.Kwani Martin Luther King hajazungumzia ndoto wakati wa enzi za ubaguzi na madhila ya kikabila?Na leo,mweusi ndie anaetawala nchini Marekani.


Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linazungumzia juhudi zilizoshindwa za Uturuki za kutaka waziri mkuu wa Danemark Rasmussen asichaguliwe kua katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya NATO.Gazezi linaandika:


"Na sisi pia tuna usemi"-Hiyo ndio sura iliyojitokeza nchini Uturuki muda mfupi kabla ya ziara ya rtais Barack Obama nchini humo.Hata baada ya kuridhia dakika ya mwisho,Rasmussen achaguliwe kua katibu mkuu wa NATO,hawakuacha kujinata."Uturuki inashinda kwa kumpa mtu mkono"-ni mojawapo ya vichwa vya maneno magazetini jana.Wahariri wamesifu ridhaa za NATO kwa serikali yao.Marekani inaihitaji Uturuki nchini Afghanistan,nchini Iran na nchini Irak pia.Wanajeshi wa Marekani watakapoihama Irak,watalazimika kwa sehemu kubwa kusalia kwanza nchini Uturuki.Kama zamani George Bush alikua akilaani maingiliano kati ya Uturuki na Iran,Barack Obama anataka kuyatumia."


Muandishi:Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman