1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama Berlin

25 Julai 2008

Hotuba ya mtetezi wa urais wa Marekani Berlin jana ilisisimua.

https://p.dw.com/p/EjYR

Mtetezi wa kiti cha urais wa Marekani, kwa niaba ya chama cha Democratic Party, seneta Barack Obama, alitoa jana hatuba ya kusisimua iliosubiriwa kwa hamu kuu.Obama aliitoa hotuba hiyo akifuata mila na desturi za marais wa zamani wa Marekani waliotembelea Berlin.

Wakaazi wa jiji la berlin, walimpokea jana Barack Obama kama jogoo lao au superstar.Magazeti ya jiji kuu la Ujerumani na maalfu ya waliokwenda kumlahki seneta Obama -mtu ambae aweza kuibuka rais anaefuta wa Marekani,walishikamanisha matumaini na ndoto zao kwa mtetezi huyu mwenye heba , wa kuvutia anaetapia wadhifa wenye mamlaka makubwa duniani.Wanatamani kupata kiongozi mpya mwenye sera tofauti kabisa na zile za George Bush,kiongozi atakaefanya yote kinyume kabisa na bora zaidi kuliko Bush aliepoteza zamani imani ya wakaazi wengi wa Ulaya.

Haya ni matarajio sasa ya kuwa na kiongozi wa kisiasa wa aina nyengine kabisa katika medani ya kisiasa na hasa kwa wale wasio na ushawishi wa kisiasa.

Seneta Obama jana alitoa hotuba kali,ya kusisimua iliojengeka kwa hoja akifuata nyayo na desturi za marais wakubwa wa Marekani waliomtangulia-JF Kennedy na Ronald Reagan.Ilikua hotuba hatahivyo ,isioashiria nyumbani (Marekani) vipi sera zake zitakua ataposhika hatamu za urais.

Aliusifu mji wa Berlin kama kituo cha uhuru na matumaini-maneno ambayo rais yeyote yule wa Marekani angeyadhukuru huko Berlin.Alikumbusha ile misafara ya ndege miaka 60 iliopita kuwasaidia wakaazi wa Berlin waliozingirwa na kwa kuwa vita baridi hivi sasa tumevipa mgongo,seneta Obama alipendekeza tujenge daraja jipya la kuwasiliana kwa waumini wa dini mbali mbali na kuzika tofauti tulizonazo katika karne hii ya 21.

Mwito wake pawepo sasa usuhuba mpya kati ya pande mbili za bahari ya Atlantik (Ulaya na Marekani), ambao utapiga vita vikali zaidi dhidi ya ugaidi kuliko ilivyofanyika hadi sasa, ni jambo lilililotazamiwa.

Na hata ikihitajika kutumia majeshi na fedha zaidi-jambo ambalo Obama hakulitaja, lakini ndio dai lake, ni dhahiri hapo hakuwapendeza wasikilizaji wake wa kijerumani.

Kwani, sehemu hii ya hotuba yake haikushangiriwa.

Kwani, ni dai ambalo lingeweza pia kutolewa na George Bush.

Na jinsi gani Mwito wa Obama wa kuwa na dunia bila ya silaha za kinuklia unavyolingana na ukweli wa mambo duniani ni jambo la kuweka shaka shaka kwa jicho kwamba nchi zaii na zaidi leo zinagombea kumiliki silaha za nuklia na kutojali ukaguzi wa kimataifa.

Kutoka Pakistan hadi Iran hali ni hiyo.Mwito wa Obama wa kuwa na sera mpya ulimwenguni ya kuhifadhi mazingira sio tu unamleta pamoja na wafuasi wake wa Ujerumani,bali hata na mpinzani wake wa chama cha republican anaegombea wadhifa wa urais-John McCain.

Hotuba ya Obama ilisisimua mno katika ile sehemu alipowataka wasikilizaji wake wa kijerumani kurejesha imani yao kwa Amerika inayotetea uhuru na haki.Kwamba Obama aliungama makosa ya Marekani,anatofautiana hapo na George Bush na hivyo ahadi yake aliotoa ya kutaka ushirika wa aina mpya na weenye dhamana kati ya washirika wa pande mbili za Atlantik (NATO) si maneno matupu.

Mtihani wa kujipatia imani na wafuasi barani Ulaya,bila shaka amepita Obama.Katika uchaguzi wa rais nchini Marekani, hapo Novemba ,wanaopiga kura ni wamarekani.Na picha kutoka Berlin,hadi wakati huo, zitakuwa zimesahaulika.