1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama hatahudhuria maandamano mjini Paris

11 Januari 2015

Rais Barack Obama hatajiunga leo Jumapili(11.01.2015)na viongozi wengine duniani katika maandamano mjini Paris wakiomboleza wahanga wa mashambulio ya wiki hii yaliyofanywa na Waislamu wenye itikadi kali nchini Ufaransa.

https://p.dw.com/p/1EIU5
Frankreich Gedemken der Opfer in Lille 10.01.2015
Maandamano mjini Paris katika mshikamano na wahanga wa shambulio la kigaidiPicha: Charlet/AFP/Getty Images

Tangu mauaji yaliyofanywa ambapo watu 12 wameuwawa katika jarida la kila wiki la vikatuni vya dhihaka Charlie Hebdo siku ya Jumatano -- na kufuatiwa na mashambulio tofauti ambayo yamesababisha watu watano zaidi kuuwawa---Obama ametoa maazimio kadhaa kuiunga mkono Ufaransa, "rafiki wa tangu zamani wa Marekani.

Lakini atajiunga na viongozi wengine ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron , kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambao wote wanatarajiwa kuhudhuria maandamano hayo. Zaidi ya watu milioni moja wanatarajiwa kuhudhuria.

Machtwechsel im US-Senat
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: picture-alliance/AP Photo/C. Kaster

Ufaransa kupambana na ugaidi

Ufaransa imeapa kupambana na ugaidi kwa kauli mbiu ya "Uhuru" katika maandamano makubwa ya mshikamano leo Jumapili(11.01.2015) baada ya siku tatu za umwagaji mkubwa wa damu ambao umeiogofya dunia.

Polisi wanamtafuta mwanamke ambaye anahusika na washambuliaji hao watatu wenye mafungamano na kundi la al-Qaeda , lakini maafisa wa Uturuki wamesema inaonekana kuwa tayari amejipenyeza nchini Syria.

Maandamano leo Jumapili pia ni changamoto kubwa ya kiusalama kwa taifa hilo lililoko katika hali ya tahadhari kwa ajili ya mashambulizi zaidi, baada ya watu 17 pamoja na watu hao watatu washambuliaji wameuwawa katika muda wa siku tatu za mashambulio dhidi ya jarida la vikatuni vya dhihaka, duka la Wayahudi na polisi mmoja na kuiweka Ufaransa kuwa nchi iliyobadilika.

Trauer nach Anschlag auf Charlie Hebdo - Solidaritätsveranstaltung in Berlin
Maandamano ya mshikamano na jarida la Charlie HebdoPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Sohn

Mamia kwa maelfu ya watu waliandamana jana Jumamosi (10.01.2015) katika miji ya Toulouse upande wa kusini , Rennes upande wa magharibi na kuonesha heshima kwa wahanga , na mji wa Paris unatarajia kufanya maandamano ambayo yatahudhuriwa na maelfu ya watu leo Jumapili katika maandamano ya mshikamano.

Misikiti na masinagogi yanalindwa

Zaidi ya polisi 2,000 wamewekwa , pamoja na mamia kwa maelfu ambao tayari wanalinda masinagogi, misikiti, shule na maeneo mengine nchini Ufaransa.

Mshikamano dhidi ya itikadi kali ni ujumbe utakaotumiwa katika maandamano ya Jumapili. Miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria ni waziri mkuu wa Israel na rais wa Palestina. Rais wa Ukraine na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, na viongozi wa Uingereza, Ujerumani, NATO, jumuiya ya mataifa ya Kiarabu na Umoja wa Afrika.

Trauer nach Anschlag auf Charlie Hebdo in Paris
Mshikamano na wahanga katika ofisi za jarida la Charlie HebdoPicha: picture-alliance/G. Van der Hasselt/Anadolu Agenc

Pamoja na wananchi wa Ufaransa, kutoka wanasiasa na pia viongozi wa dini.

Maafisa wa ngazi ya juu wa usalama wa Ulaya na Marekani pia wanakutana katika mkutano wa dharura mjini Paris juu ya kupambana na ugaidi.

Maandamano hayo "yanapaswa kuonesha nguvu, heshima ya watu wa Ufaransa ambao watapiga kelele kutokana na mapenzi yao kwa uhuru na uvumilivu," waziri mkuu Manuel Valls amesema siku ya Jumamosi.

"Waandishi habari wameuwawa kwasababu wanatetea uhuru. Polisi wameuwawa kwasababu walikuwa wakikulinda. Wayahudi wameuwawa kwasababu walikuwa Wayahudi," amesema. "Uchungu na hasira unapaswa kuendelea kwa ukamilifu - sio kwa siku tatu pekee, bali wakati wote.

Trauer nach Anschlag auf Charlie Hebdo - Solidaritätsveranstaltung in Berlin
Maombolezo katika ofisi za Charlie Hebdo mjini ParisPicha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Al-Qaeda wanahusika

Tawi la al-Qaeda nchini Yemen limesema limeongoza shambulio la Jumatano dhidi ya jarida la Charlie Hebdo kulipza hadhi ya mtume Muhammad, lengo la kila mara la jarida hilo la kila wiki la vikatuni vya dhihaka.

Lengo la msako wa polisi kwa sasa unaelekezwa kwa mjane wa Coulibaly , Hayat Boumeddiene. Polisi wamemtaja kuwa mshirika wa mume wake katika shambulio dhidi ya polisi wa kike na huenda ana silaha.

Paris Geiselnahme Supermarkt Polizei 09.01.2015
Polisi wakielekea kupambana na wateka nyara katika dula la Wayahudi mjini ParisPicha: Reuters/Y. Boudlal

Lakini afisa wa ujasusi nchini Uturuki ameliambia shirika la habari la Associated Press jana Jumamosi kwamba mwanamke ambaye ana jina kama hilo amekwenda Sabiha Gokcen, ambao ni uwanja wa ndege wa pili mjini Istanbul, Januari 2, na kwamba anafanana na picha iliyosambazwa ya boumeddiene.

Uwangaji damu nchini Ufaransa unaweza kuashiria mwanzo wa wimbi la mashambulizi katika bara la Ulaya, kwa mujibu wa mawasiliano ya viongozi wa kundi la Dola la Kiislamu yaliyonaswa na maafisa wa ujasusi wa Marekani, gazeti la Bild nchini Ujerumani limesema leo Jumapili(11.01.2015).

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape

Mhariri: Sudi Mnette