1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama na waafrika Ujerumani

23 Julai 2008

Seneta barack Obama anawasili Ujerumani leo na atahutubia mjini Berlin.Waafrika wa Ujerumani waionaje ziara yake ?

https://p.dw.com/p/EiX3

Seneta Barack Obama,anatazamiwa kuwasili leo Ujerumani na kuhutubia mjini Berlin kutoka nguzo mashuhuri ya ushindi-kiasi cha maili 1 kutoka Lango la kihistoria la Brandeburger Tor.

Waafrika waishio Ujerumani wanamuangalia kwa jicho gani Barrack Obama, ambabe mbaba yake ni wa asili ya Kenya ?

Siraj kalyango anaripoti:

►◄

"Sisi tunajitambulisha kabisa na Obama.Takriban wote wenye mizizi na Afrika ,wameingiwa na shauku mno." Alinukuliwa muafrika mmoja aitwae Patrice Kissasse kusema .

Mkongomani huyo anapanga pamoja na marafiki zake kufunga safari leo hii kwenda katika "SIEGESÄULE" -ile nguzo ya ushindi mjini Berlin, ili kumuona na kumsikia mtetzezi huyu mwenye asili ya Kenya anaetetea wadhifa wa kiti cha urais cha Marekani.

Obama -anaongeza Mkongomani huyo,itampasa kushughulikia kuwa madikteta baryani afrika kama vile Robert Mugabe nchini Zimbabwe hawan'gan'ganii tena kusalia madarakani.

"Hili ni jambo muhimu kabisa kufanya kwa bara la Afrika ."-alisema Patrice Kissasse.

Kila upitapo katika jamii ya wajerumani wenye asili ya kiafrika ,soga limetuwama wakati huu ju ya Barack Obama kama anvyosema Patrice.Pekee kuwa muamerika mweusi anagombea wadhifa wa urais wa marekani ,anaona ni jambo la kufurahisha ajabu.

Wahamiaji na watoto waliochanganya damu ya kiafrika na kijerumani humu nchini, wanahisi wamethaminiwa na wametiwa mori kujitahidi nao kusonga mbele.

Mkongomani huyo lakini mbali na shauku kubwa alionayo hakusahau kujizuwia kidogo.Anasema kwa bahati mbaya wamarekani wangehiyari kumuona mwanamke mweupe akiingia Ikulu kuliko mwanamume mweusi.

Hata Roland Prejawa,mwenyekiti wa Umoja wa Berlin kwa afrika ambamo unajumuisha waghana,wakamerun,wasenegal,wanigeria na wakongomani ,rais mwenye asili ya kiafrika nchini marekani atalisaidia zaidi bara la Afrika kujikomboa.

Kwa jinsi alivyoona yeye kuna shauku kubwa miongoni mwa waafrika nchini Ujerumani,lakini shauku yao hiyo ina mpaka wake.

kuna hofu kwamba, akichaguliwa rais huko Marekani atatawala akivaa soksi nyeupe mkononi.Waafrika wa Ujerumani hawamuangalii seneta Obama kama mkombozi wao bali watamkaribisha mikono miwili.

Hata familia moja ya Msenegal na mjerumani Amberg-Gueye katika mkoa wa Bavaria imeamua kuiangalia kwa hamu kuu ziara ya Bw.Obama hii leo."Akiwa mtoto wa mama mzungu na baba muafrika ,Obama aweza kuwakusanya binadamu wote pamoja.

Ikiwa atafaulu hivyo itakua uzuri kabisa."Amadou Gueye pamoja na mkewe wa kijerumani Alice Amberg wasnapanga kumchukua mtoto wao kutoka kambi yake ya likizo huko aliko ili waende leo berlin kumshangiria Barack Obama.kwani, mtoto wao huyo akitaka kwa kila hali kumuona kwa macho yake barack Obama.

kwani, familia hii ilivutiwa mno na hotuba alioitoa mapema mwaka huu seneta Obama aliponadi, " Kwa miaka mingi sasa hakujakuwa na badiliko lolote katika swali la kuondosha hisia za kikabila."

Watoto wetu walisoma hotuba yake hiyo ya kampeni ya uchaguzi kwa tafsiri yake ya kijerumani na walivutiwa mno-alisema bibi Amberg.

Sasa kuna mtu mweusi anaeheshimika kama msomi na sio kwa sifa zake kama ni mwanaspoti mashuhuri,mwanamuziki maarufu au avutia tu kwa umbo na heba yake.