1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama sasa anakaribia ushindi wa kuwa mgombea.

21 Mei 2008

Ni baada ya matokeo ya Kentucky na Oregon.

https://p.dw.com/p/E3m3
Hilary Clinton na Barack Obama ,wanaogombea uteuzi wa chama chao cha Democratic.Picha: AP

Kufuatia uchaguzi wa mwengine wa awali wa kumtafuta atakaekua mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic nchini Marekani, Barack Obama amesema sasa anakaribia kufikia hatua kubwa mpya katika kuwania nafasi hiyo dhidi ya mpinzani wake Hilary Clinton, ikiwa ni baada ya matokeo chaguzi za jana, ambapo Bibi Clinton alinyakua ushindi katika jimbo la kusini la Kentucky na Obama kushinda huko Oregon.

Obama anayepigania kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani anajiwekea matumaini makubwa ya kupata ueuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wake baada ya kujihakikishia uungaji mkono zaidi wa wajumbe. Aliwaambia wafuasi wake waliokua wakimshangiria " Obama 2008" kwa kusema sasa wamesogea mbali wakikaribia kupata uteuzi wa chama chao kuwania urais wa Marekanina kuongeza,"Huenda safari yetu ikawa ndefu, kazi yetu ikawa kubwa, lakini ndani ya nyoyo zetu tuko tayari kwa mabadiliko."

Wachambuzti wanasema hivi sasa nafasi ya Bibi Clinton licha ya ushindi wake mkubwa katika jimbo la Kentucky sasa itategemea tu maafisa karibu 800 wa chama kubadili upande watakapopiga kura kwenye mkutano mkuu mwezi Agosti.

Lakini pamoja na hayo Seneta huyo mwenye umri wa miaka 60 ameahidi kuendelea kuipa matumaini ndoto yake ya kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Marekani, kwa kusubiri matokeo ya uchaguzi mwengine tena wa awali wa Wademocrats Juni 3. Baada ya ushindi wa Kentucky aliwashukuru wafuasi wake akisema,"Leo tumejipatia ushindi muhimu."

Bibi Clinton akaongeza kwamba ataendelea na kinyanganyiro hicho hadi mgombea ameueuliwa, akiopuuza wito wa baadhi ya vigogo chamani kwamba sasa wakati umewadia kujiengua na kumuachia Obama.

Kwa upande mwengine wagombea wote wawili, wametoa taarifa ya kumtakia nafuu na afya njema, mawanasiasa mkongwe wa chama cha Democrats Seneta Edward Kennedy ambaye alikimbizwa hospitali hapo juzi na sasa madaktari wanasema wamegua kwamba anauvimbe kwenye sehemu moja ya ubongo. Taarifa ya kumuombea afya njema imetolewa pia na anayetarajiwa mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi ujao Novemba Seneta John Mccain. Edward Kenny mwenye umri wa miaka 76 ndiye pekee aliyebaki hai miongoni mwa ndugu watatu wa kiume waliogeuka kuwa maarufu katika siasa za marekani kutoka familia ya Kennedy. Kaka zake wawili John F. Kennedy aliyekua rais na Robert Kennedy waliuwawa.

Kwa upande mwengine utafiti wa kura ya maoni miongoni mwa wamarekani uliofanywa na shirika la habari la Reuters na taasisi ya Zogby umeonyesha kwamba Obama kwa sasa anamtangulia McCain kwa asili mia 48 dhidi ya 40.Sambamba na hayo uatafiti huo pia umegundua kwamba Obama anaongoza mbele ya mpinzani wake chjama bibi Clinton kwa asili mia 26, ikiwa ni ongezeko la maradufu ikilinganishwa na mwezi uliopita, huku dalili zikionyesha kwamba iwapo mkondo huo utaendelea, basi ana nafasi nzuri ya kumenyana ana Mrepublican McCain mwezi Novemba.