1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ODM yafuta mandamano ya jumanne

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClZC

NAIROBI:

Chama cha upinzani nchini Kenya cha Orange Democratic Movement-ODM-kimefuta mikutano pamoja na maandamano kilichokuwa kimeyapanga kufanyika jumanne.

Hatua ya kufuta maandamano hayo imekuja wakati wapatanishi wa kimataifa wakiwasili huko kutafuta njia za kumaliza mgogoro nchini humo.

Serikali ambayo hapo mapema ilikuwa imepiga marufuku mikusanyiko yote ya kisiasa,imekaribisha uamuzi huo.Msemaji wa chama cha ODM –amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na kutarajiwa kuwasili nchini humo kwa mkuu wa Umoja wa Afrika rais wa Ghana Bw John Kufour.

Wakati huohuo afisa wa ngazi za juu wa Marekani ameanza juhudi za upatanishi.

Watu wasiopungua 300 walifariki ilhali wengine zaidi ya laki mbili kuachwa bila makazi kufuatia ghasia za kikabila zilizosababishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi Desemba 2007 ambao ulimrejesha madarakani Rais Mwai Kibaki.