1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oliver Kahn kuwa meneja wa Schalke ?

20 Machi 2009

Kipa wa zamani wa Taifa wa Ujerumani ashika wadhifa mpya ?

https://p.dw.com/p/HG7c
Oliver KahnPicha: AP

Viongozi wa Bundesliga Hertha Berlin wanakabiliwa leo na changamoto kubwa huko Stuttgart ingawa wanajua watab akia kileleni mwa Ligi wakishinda au wakishindwa hii leo.Mapambano 8 tu ya Bundesliga yakisalia kukamilisha msimu,Hertha timu ya jiji kuu Berlin,inaingia uwanjani leo ikiongoza kwa pointi.

Kipa wa zamani wa Taifa na mabingwa Bayern munich Oliver Kahn amethibitisha kuwa anashauriana wakati huu na Schalke kuwa meneja wa timu hiyo.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza,mabingwa manchester united ambao wameanza kutoa shaka shaka ya kutimiza shabaha yao ya vikombe 5 msimu huu baada ya kukandikwa mabao 4-1 na Liverpool mwishoni mwa wiki iliopita, wana miadi leo na Fulham.Liverpool inarudi uwanjani kesho ikitazamia kutamba nyumbani mbele ya Aston Villa.

Hertha Berlin inaongoza Bundesliga kwa pointi 4 ikiandamwa na mabingwa Bayern Munich,Wolfsburg na Hamburg. Stuttgart leo haimudu pigo jengine kutoka Berlin baada ya jumapili iliopita kuadhibiwa kwa mabao 4 :0 na Werder Bremen -timu ya kwanza wiki hii iliokata tiketi yake ya duru ijayo ya Kombe la ulaya la UEFA.

Nahodha wa Hertha Berlin, Arne Friederich alisema baada ya timu yake ya Berlin kuilaza Leverkusen kwa bao 1:0, kuwa "ndoto yaoya kutwaa ubingwa inaendelea".

Ndoto pia wanayo bado mabingwa Bayern Munich na kocha wao Jurgen klinsmann. Bayern Munich inaweka ndoto tangu ya kutwaa tena Kombe la Ulaya la klabu bingwa-champions League hata ya taji la Bundesliga licha ya misukosuko yake .

Munich inacheza nyumbani leo na Karlsruhe inayoburura mkia wa ligi.Na baada ya kutamba katika mechi 3 zilizopita -mabao 7-1 dhidi ya sporting Lisbon ya Ureno katika champions League,mabao 5-1 katika lango la Hannover na mabao 3-0 ilioikomea Bochum,Bayern munich inalinyatia tena taji tangu la Bubdesliga hata la ulaya.

Katika changamoto nyengine, Energie Cottbus inaikaribisha nyumbani , FC Cologne inayohitaji ushindi mwengine baada ya kulazwa kwa mabao 4-2 na Borussia Moenchengladbach mwishoni mwa wiki iliopita.Kesho,macho yanakodolewa mpambano moja wa kukata na shoka:

Schalke inaumana nqa Hamburg. Taarifa zinasema Schalke inazungumza na kipa wa zamani wa Taifa na wa Bayern Munich Oliver Kahna aewe meneja wake.Kahn amekutana na mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Schalke Clemens Toennies wiki tu baada ya Schake kumtimua meneja wake Andreas Mueller.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza kocha wa Chelsea ambae wakati huo huo ni kocha wa Urusi, mdachi Guus Hiddink, alisema jana kwamba, yamkini akabakia kuwa kocha wa Chelsea mjini London ikiwa Urusi,itashindwa kukata tiketi ya Kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini.Hiddink alichukua uongozi wa Chelsea baada ya kutimuliwa kocha mbrazil Felipe Scolari lakini kwa kipindi kifupi tu.

Chelsea inacheza leo na Tottenham Hotspur wakati mabingwa M anchester United wanakumbana na Fulham .

Liverpool inayoendelea kutoa changamoto kwa Manu ina miadi kesho na Aston villa.Arsenal inaitembelea leo Newcastle United wakati Potsmouth inachuana na Everton.Stoke City inacheza na Middlesbrough.

Muandishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Aboubakary Liongo