1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olmert aondoa uwezekano wa kusitisha mapigano na Hamas.

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfdq

Jerusalem.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameondoa uwezekano wa kusitisha mashambulizi na kundi la wapiganaji wa Hamas , akisema kuwa jeshi litaendelea kushambulia wapiganaji wanaofyatua makombora dhidi ya Israel kutoka katika eneo la ukanda wa Gaza. Olmert amesema hakutakuwa na usitishwaji wa mapigano hadi pale Hamas wanakapokubali masharti yaliyowekwa na kundi la pande nne linalofanya majadiliano kuhusu mashariki ya kati. Kundi hilo linaloundwa na Marekani, umoja wa Ulaya , Russia na umoja wa mataifa, limedai kuwa Hamas iitambue Israel, iachane na matumizi ya nguvu na kufuata makubaliano yaliyopo ya amani. Mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza yameuwa zaidi ya wapalestina 20 katika wiki chache zilizopita.

Hamas walichukua udhibiti wa eneo hilo Juni mwaka huu baada ya kuwaondoa wanajeshi wanaomuunga mkono rais wa Palestina Mahmoud Abbas.