1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olmert ataka Iran ishinikizwe zaidi

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6ZP
Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa iishinikize zaidi Iran. Baada ya mkutano wake na kansela wa Ujerumani Angela Merkel, waziri mkuu Olmert amesema ipo haja ya kutafakari njia zinazoweza kutumiwa kuumaliza mzozo wa nyuklia wa Iran. Olmert amesema anaamini serikali ya mjini Tehran inatengeneza kwa siri bomu la nyuklia. Kiongozi huyo pia amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wanamgambo wa kipalestina wanaofanya mashambulio ya maroketi kutoka Ukanda wa Gaza. Kansela Merkel kwa upande wake amezungumzia juu ya changamoto kubwa zinazoukabili mchakato wa kutafuta amani katika Mashariki ya Kati. Amesema muda wa kufanya mazungumzo unatoweka na ipo haja ya kufanya mashauriano kwa dharura. Ujerumani inaunga mkono suluhisho litakalosababisha kuundwa kwa mataifa mawili ya Israel na Palestina.