1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olmert azuru Ujerumani

11 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D5fN

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, leo atalitembelea jumba la makumbusho ya kiyahudi mjini Berlin akiwa katika ziara yake rasmi ya siku tatu hapa Ujerumani.

Olmert atajionea vitu vya kale na stakabadhi zinazodhihirisha kuwepo kwa jamii ya wayahudi katikati mwa Ulaya kwa miaka 2000 iliyopita.

Ehud Olmert aliwasili jana jioni mjini Berlin na anatarajiwa kukutana na kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na rais Horst Kohler hapo kesho.

Kiongozi huyo wa Israel atakamilisha ziara yake ya humu nchini hapo kesho.