1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oman kuhudhuria mkutano wa Annapolis

23 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSTP

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Nchi za Kiarabu wanakutana mji mkuu wa Misri,Cairo. Mawaziri hao wanajadili mkakati wa kuhudhuria mkutano wa amani ya Mashariki ya Kati uliopangwa kufanywa juma lijalo nchini Marekani.

Suala ni iwapo nchi za Kiarabu zitawasilishwa kwa pamoja au kama taifa moja moja.Oman imeshasema kuwa itahudhuria mkutano wa juma lijalo mjini Annapolis,Marekani,wakati nchi zingine kama vile Saudi Arabia zikisita kwa sababu hazitaraji mafanikio makubwa kwenye mkutano wa juma lijalo.