1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OPEC kupunguza utoaji mafuta

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/Fcw1

Vienna:

Rais wa Shirika la nchi zinazosafirisha mafuta kwa wingi OPEC Chakib Khelil amesema Shirika hilo litaamua kupunguza kiwango cha utoaji mafuta wakati wa mkutano wake Ijumaa ijayo. Mkuu huyo wa la Shirika OPEC amesema shirika hilo halina budi kuzingatia kile alichokiita" upunguzaji mkubwa", kutokana na kupungua kwa mahitaji kwa sababu ya mzozo wa fedha. Bw Khelil alisema utoaji mafuta unaweza ukapunguzwa kwa kiwango cha mapipa milioni mbili kwa siku. Mwanzoni mwa mwezi uliopita wa Septemba, OPEC iliweka kiwango cha karibu mapipa milioni 29 tu kwa siku. Bei ya mafuta imeshuka katika miezi ya karibuni na wiki iliopita ilianguka hadi chini ya dola 70 kwa pipa, kutoka dola 147 mwezi Juni. Kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta, Shirika la OPEC limeisogeza mbele tarehe ya mkutano wake uliokua awali ufanyike mwezi ujao.