1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni Euphrates yaendelea syria

Admin.WagnerD2 Septemba 2016

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki leo ameyapuuzilia mbali madai ya kwamba wapiganaji wa Kikurdi kwa upande wa Syria wamerejea nyuma upande wa mashariki, ya Mtoto Euphrates kaskazini mwa Syria.

https://p.dw.com/p/1Juk0
Türkische Soldaten auf einem Panzer bei der Rückkehr von einem Einsatz in Syrien
Majeshi ya Uturuki yakiwa katika operesheni nchini SyriaPicha: picture-alliance/dpa/E.Ozdemir

Awali Uturuki ililionya kwamba itaendelea kulivurumishia makombora kundi hilo la wanamgambo wa Kikurdi lijulikanayo kama-Kuridish People's Protection Units (YPG), ambalo serikali ya Ankara inalitazama kama kundi la kigaidi, lenye kuunganishwa na makundi ya waliojitenga kama halitakwenda upande wa Mashariki.

Rais Erdogan amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa akikanusha kwa kusema "Hivi sasa watu wanasema wameelekea upande wa mashariki lakini sisi tunasema hapana, hawajavuka," Alisema kiongozi huyon katika hotuba yake.

Serikali inafuatilia hali ya mambo katika mto Euphrates

Aidha Erdogan aliongeza kusema serikali yake itapata taarifa kama wanamgambo hao wataondoka katika eneo hilo. Kimsingi lengo la serikali ya Uturuki dhidi ya kundi hilo la YPG ni kuzua makundi ya wanamgambo kujiunga katika eneo linalodhibitiwa na Wakurdi katika upande wa magharibi mwa mto Euphrates, jambo ambalo Uturuki inaohofia itasababisha eneo lenye utawala wake, au mamlaka yake yenyewe nchini Syria na kuimarisha uasi katika eneo hilo la mpakani la Uturuki.

Syrien Dscharabulus Amarne FSA Kämpfer
Muungano wa majeshi katika operesheni dhidi ya IS, SyriaPicha: picture-alliances//AA/C. Ozdel

Katika hotuba yake hiyo Rais Erdogan amesema hakuna yeyote anawategemea wao kutia nafasi ya uwanja wa kuhimarishwa ugaidi. Hawawzi kuruhusu jambo hilo akitolea mfano hamasa ya makundi matatu ya Kikurdi ya Syria kuungana kaskazini mwa taifa hilo.

Tatizo la Wakurdi wa Ututuki

Wakudi kwa upande wa Uturiki nao ni tatizo lingine, kwa kugubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati huu ambapo kwa pamoja Marekani na Uturuki zikifanya jitihada za kulikomboa eneo linadhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu kwa kuyaunga mkono baadhi ya makundi.

Kundi la Kikurdi la YPG kwa mfano linaungwa mkono na Marekani ambayo imewapa mafunzo na vifaa vya kukabiliana na kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria. Juma moja lililopita jeshi la Uturuki lilianzisha operesheni kubwa katika kustawisha hali ya usalama katika eneo la mpakani ambalo kumekuwepo na wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu, pamoja na kudhibiti kusonga mbele kwa kundi la Kikurdi la YPG, ambalo linatazwamwa na Marekani kana kama muhimu katika kudhibiti makundi ya wenye itikadi kali.

Mapema Alhamis, serikali ya ilisema imesafisha vijiji kadhaa walivyoviita vya kigaidi baada ya kulidhibiti eneo muhimu la mpakani la mji wa Jarabulus pasipo kupata upinzani mkubwa. Na katika operesheni ya Euphrates, Uturuki vilevile imevurumisha makombora dhidi ya Wakurdi wa YPG. Uturuki inalitazama kundi hilo kama lenye muungano na chama cha wafanyakazi wa kikurdi PKK ambalo wimbi lake la uasi limesababisha zaidi ya watu 40,000 kupoteza maisha tangu 1984.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef