1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni kuu dhidi ya ngóme ya Wataliban

8 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZ1a

Vikosi vya Afghanistan na vikosi vya kimataifa ISAF vinavyosaidia kulinda usalama nchini humo, vimeanzisha operesheni kuu ya kuuteka mji wa Musa Qala unaodhibitiwa na wanamgambo wa Taliban tangu miezi 10 iliyopita.Majeshi ya ISAF yanayoongozwa na NATO yamethibitisha kuwa vikosi vyake viliteremshwa ukingoni mwa Musa Qala katika matayarisho ya operesheni hiyo.

Siku ya Ijumaa,vikosi vya Afghanistan na Uingereza vilitumia silaha nzito kushambulia vituo vya Taliban ukingoni mwa Musa Qala.Tangu kudhibitiwa na Taliban,mji huo umekuwa kituo kikuu cha biashara ya madawa ya kulevya katika wilaya ya Helmand,kusini mwa Afghanistan ambako afyuni ni kilimo kikuu.