1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni kuu Irak dhidi ya al-Qaeda

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cxvb

BAGHDAD:

Waziri Mkuu wa Irak,Nuri al-Maliki amesema,majeshi yake yameanzisha operesheni muhimu dhidi ya wanamgambo wa al-Qaeda.Alipozungumza mjini Karbala,al-Maliki alisema,vikosi vya Irak vimepelekwa mji wa Mosul ulio kaskazini mwa nchi kuteketeza ngome kuu ya mwisho ya waasi wa Kisunni.

Serikali ya Irak inawalaumu wapiganaji wa al-Qaeda kwa mripuko mkubwa uliotokea mjini Mosul siku ya Jumatano na kuua hadi watu 35.Shambulizi hilo pia liliwajeruhi kama watu 200 wengine.

Maafisa wa majeshi ya Marekani wanasema,magaidi wa al-Qaeda wamejikusanya upya katika mikoa ya kaskazini baada kufukuzwa kwa nguvu kutoka wilaya ya magharibi ya Anbar na mjini Baghdad.