1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OTTAWA: Serikali ya Canada kumlipa fidia Maher Arar aliyezuiliwa kimakosa kwa tuhuma za ugaidi.

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXg

Serikali ya Canada imekubali kumlipa raia wa nchi hiyo mzaliwa wa Syria fidia ya Euro karibu milioni sita nukta tisa kwa kumtuhumu kimakosa kwa ugaidi.

Maher Arar alikaa gerezani nchini Syria kwa muda wa mwaka mmoja ambapo anadai aliteswa kabla ya kuhamishiwa Marekani mwaka 2002.

Maher Arar alikamatwa katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy mjini New York alipokuwa akirejea nchini Canada kutoka likizoni.

Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper alimtaka radhi hadharani Maher Arar ambaye ingawa aliridhia lakini alisema maisha yake yamevurugika tangu alipokamatwa.