1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OUGADOUGOU: Gbagbo na Soro kutia saini makubaliano ya amani ya Ivory Coast

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMZ

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast na kiongozi wa waasi Guillaume Soro leo hii wanatia saini makubaliano yenye lengo la kukomesha mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe nchini humo.Makubaliano hayo yalipatikana siku ya Jumamosi chini ya usimamizi wa Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso.Desemba mwaka jana,Rais Gbagbo alipendekeza kuwa na mazungumzo ya uso kwa uso kwa azma ya kuzindua utaratibu wa amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi.