1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OUGADOUGOU: Makubaliano yatiwa saini kufufua mchakato wa amani Ivory Coast

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMS

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast na kiongozi wa waasi Guillaume Soro,leo hii wametia saini makubaliano yenye lengo la kufufua mchakato wa amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi iliyogawika.Makubaliano hayo ni matunda ya mwanzo ya majadiliano ya uso kwa uso yaliyozinduliwa mwanzo wa mwezi Februari katika mji mkuu wa Burkina Faso.Makubaliano hayo yalipatikana siku ya Jumamosi chini ya usimamizi wa Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso.