1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pakistan yafanya majaribio ya kombora lake lenye uwezo wa kubeba kichwa cha Nuklia

1 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D15g

ISLAMABAD:

Jeshi la Pakistan linasema kuwa,limefaulu kufanya majaribio ya kombora la masafa marefu lenye uwezo wa kubeba Nuklia katika juhudi za kuimarisha ulinzi wa nchi hiyo.

Hilo ndilo jaribio la pili kufanyika katika kipindi cha wiki moja.Kombora hilo linauwezo wa kwenda umbali wa kilomita 1,300.Jaribio hilo limehudhuriwa na rais Perves Musharraf.Taarifa ambayo imetolewa na jeshi imenukuu rais akipuuzia mbali madai kuwa silaha za Nuklia za Pakistan zaweza kuanguka katika mikono ya waislamu wenye msimamo mkali.Amesema kuwa hofu hizo hazina msingi na zinatolewa na wale wanaoitakia mabaya Pakistan.India ambayo nayo ina Nukila imekuwa ikifanya majaribio kadhaa ya makombora yake na nchi kila mara nchi hizo mbili zimekuwa zikiarifiana mapema kuhusu majaribio yao.