1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pakistan yatakiwa kuwa karibu na jumuiya ya madola.

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTGL

Kampala.Viongozi wa jumiya ya madola Commonwealth wameitaka Pakistan jana kuendelea kuhusiana na kundi hilo wakati wakikamilisha mkutano wao mjini Kampala ambao umesitisha uanachana wa nchi hiyo inayoongozwa na jenerali Pervez Musharraf. Viongozi kutoka jumuiya hiyo ya mataifa 53, wameitaka Pakistan kulichukulia suala la jumuiya hiyo kuitaka kuendelea kuhusiana kwa njia nzuri , ili kusaidia kurejeshwa kwa serikali ya kidemokrasia na utawala wa kisheria.

Viongozi hao wameidhinisha uamuzi wa siku ya Alhamis wiki iliyopita uliotolewa na mawaziri wa mambo ya kigeni wa jumuiya ya commonwealth kuiondolea kwa muda uanachama Pakistan , baada ya Musharraf kushindwa kufikia muda wa mwisho wa siku kumi kumaliza hali ya hatari, licha ya hatua kadha zilizopigwa katika maeneo mengine. Pakistan imeuita uamuzi huo wa kusitisha uanachama kuwa usiokuwa na maana na usiostahili na kutishia kujitoa kabisa kutoka katika jumuiya hiyo, kama ilivyofanya Zimbabwe.