1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pande zinazozozana za Sudan zinafanya uhalifu Darfur-ICC

Bruce Amani
30 Januari 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imeliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, wamebaini kuna misingi ya uhalifu uliofanywa na jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF eneo la Darfur katika vita vya nchini humo.

https://p.dw.com/p/4boni
ICC | Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai  Karim Khan
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC Karim KhanPicha: Chepa Beltran/LongVisual via ZUMA Press/picture alliance

Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai - ICC Karim Khan ambaye hivi karibuni alizuru nchi jiraniChad ambako maelfu ya watu kutoka Darfur wamepewa hifadhi, ameonya kwamba wale aliokutana nao katika kambi za wakimbizi wanahofia kuwa Darfur itakuwa kile wanachokiita "ukatili uliosahaulika."

Soma pia:Mapigano Sudan Kusini yaua zaidi ya watu 50

Ameihimiza serikali ya Sudan kuwapa maafisa wake wa upelelezi visa za kuingia nchini humo na kuyashughulikia maombi 35 ya msaada.