1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa amaliza ziara yake Uingereza

19 Septemba 2010

Ziara ya Papa Benedict Uingereza imekumbwa na maandamano, kuhusiana na kashfa ya ngono iliyoikumba Kanisa Katoliki.

https://p.dw.com/p/PFzj
Pope Benedict wa 16, amalia ziara yake Uingereza.Picha: AP

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict wa 16 anamaliza ziara yake nchini Uingereza Jumapili hii kwa kumfanya mtakatifu Kadinal John Henry Newman wa Karne ya 19,Muanglikana aliebadili madhehebu na kuwa Mkatoliki. Misa hiyo itafanyika katika uwanja wa wazi, huko Birmingham.  Marehemu Kadinali Newman msomi ambaye alikuwa kasisi alikuwa mmoja waliongoza vuguguvu la Oxford ambalo lilianzisha itikadi za Kikatoliki katika kanisa la Kianglikana. Hapo jana Papa Bendict alikutana na wahanga wa vitendo vya unyanyasaji wa kingono vilivyofanywa na mapadri wa kanisa hilo, na kuelezea aibu na huzuni yake kutokana na mateso waliyoyapata wahanga hao.Maelfu waliandamana kupinga ziara hiyo ya Papa kwa namna alivyoshughulikia kashfa ya ngono iliyoikumba Kanisa Katoliki.

Wakati huo huo polisi nchini Uingereza wamewaachilia huru watu sita waliokamatwa kwa tuhuma kwamba walikuwa na njama ya ugaidi dhidi ya Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani. Watu hao waaliachiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka yeyote.