1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedikt XVI kuwasili Benin leo

18 Novemba 2011

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedikt XVI anaianza leo ziara nchini Benin. Kanisa katoliki limekuwa na jukumu kubwa katika kuimarisha imani za wakristo wa bara zima la Afrika.

https://p.dw.com/p/13Cof
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedikt wa 16Picha: AP

Katika ziara yake hii ya pili Afrika, Papa Benedikt XVI atawasilisha kwa maaskofu wa bara zima rasimu iliyobuniwa mwaka 2009 kama muongozo, wakati huu yamekuwa yakishuhudiwa mabadiliko makubwa. Hasa maendeleo yasolingana, rushwa, upotevu wa maadili, kudhoofika kwa tawala za kijadi, pamoja na ushindani kutoka kwa makanisa ya kiprotestanti.

Ni katika mji wa Ouidah umbali wa kilomita 40 kutoka mji mkuu Cotonou, karibu na kaburi la kardinali Bernardin Gantin mmoja wa waasisi wa sera ya ukristo wa kiafrika, aliyefariki mwaka 2008, ndipo baba mtakatifu huyo atasaini kitabu hicho cha muongozo, baada ya kujadiliana na viongozi wa kidini wa nchi hiyo.

Markt in Cotonou, Benin
Soko la mji wa Cotonuo, BeninPicha: AP Photo

Mji huo wa pwani uliteuliwa kwa makusudi mazima kwanza ndiko walikofikia wamisionari wazungu wa kwanza miaka 150 iliyopita, na hivyo kujengwa sehemu hiyo chuo kikuu cha kikatoliki cha Afrika magharibi. Na pia ni katika mji huo kulikoanzia biashara ya watumwa kuelekea sehemu nyingine za dunia. Na hatimaye mji wa Ouidah ni moja ya vitovu vya Voudou madhehebu ya jadi katika eneo hilo la Afrika.

Mjini Cotonou kiongozi huyo wa kanisa katoliki atatembelea kituo cha wamisionari wa mama Teresa, na wakuu wa dini nyingine na kukutana na wajumbe wa serikali ya Benin kabla ya kuongoza ibada ya misa kwenye uwanja wa urafiki.

Wakristo milioni 3 wa Benin sawa na asilimia 34 ya raia jumla wa nchi hiyo, na wengine kutoka nchi jirani wamejiandaa kumpokea papa kwa shangwe.

Alipolitembelea bara la Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 2008, katika ziara iliyomfikisha katika nchi za Angola na Cameroon, " Papa alishuhudia imani ya dhati katika jamii inayokumbwa na mageuzi, " alisema Mario Giro kutoka shirika la Saint Egidio, mpatanishi katika migogoro mingi ndani ya nchi za Afrika.

Papst Benedikt in Kamerun
Papa Benedikt XVI alipokuwa ziarani Cameroon mwaka 2008Picha: AP

" Papa akusudia kutoa shime kwa imani ya waafrika, na kuliwezesha kanisa kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo," aliongeza kusema.

Mchambuzi mmoja nchini Benin alisema "Papa anasubiriwa kwa hamu kubwa, kurejesha nidhamu ndani ya nyumba."

Maaskofu wawili akiwemo yule wa mjini Cotonou, Marcel Hanorat Agboton, walifutwa kazi kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na rushwa, mapadiri wanaoishi na wake, na mikasa inayowahusisha na wasichana wenye umri mdogo, pamoja na wakatoliki wengi ambao pia ni wafuasi wa madhehebu ya jadi.

Benin inayotambulika kama "mtaa wa kilatino" Afrika, ina viongozi wazuri wa kikristo waliofuzu kutoka kwa wamisionari, walikuwa na jukumu katika kuwezesha kufanikiwa  kipindi cha mpito kuelekea demokrasia baada ya kumalizika utawala wa kijeshi. Hasa Askofu mkuu Isidore de Souza aliyeongoza kongamano la kitaifa mwaka 1990.

Hata hivyo kanisa katoliki limekuwa likijikuta likikabiliwa na upinzani. Ushawishi wa siri ila unao kuwa wa Uislam, licha ya kuwa waumini wa dini hizo mbili bado wanatangamana. Pia kumekuwa na ongezeko kubwa la makanisa ya kiprotestanti yanayopendekeza imani rahisi, inayoahidi pepo kwa kutoa sadaka.

"Watu wanakabiliwa na njaa wanamtega sikio wa kwanza kuwafikia lakini baadaye hurejea kwenye kanisa katoliki," lisema msomo mmoja wa dini.

Mwandishi: Amida ISSA/afp

Mhariri: Josephat Charo.