1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedikti XVI atembelea mahala pa hujuma ya kigaidi New York.

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DlAU

New York:

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedikt XVI, anamaliza ziara yake ya siku tano nchini Marekani leo. Muda mfupi uliopita aliwasili katika uwanja wa Ground Zero, mahala palipofanyika mashambulio ya kigaidi kwenye jengo la kituo cha biashara duniani Septemba 11, 2001na kuomba amani.Kiongozi huyo aliwasili kukiwa na ulinzi mkali. Papa Benedikt ambaye ni kiongozi wa kwanza wa kanisa katoliki duniani kuzuru mahala hapo, alikutana pia na walionusurika pamoja na familia za waliouwawa katika mashambulio hayo.Kabla ya kuondoka ataongoza misa kubwa katika uwanja wa michezo wa Yankee na ataagwa baadae katika hafla maalum kwenye uwanja wa ndege na Makamu wa rais wa Marekani Dick Cheney.