1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis akutana na jamaa za waliotekwa na Hamas

22 Novemba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani papa Francis leo amekutana na jamaa za mateka wa Israel huko Gaza na wafungwa wa Palestina walioko Israel, akisema pande zote mbili zinakabiliwa na mateso.

https://p.dw.com/p/4ZKTx
Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa FrancisPicha: Riccardo De Luca/Anadolu/picture alliance

Papa Francis amebainisha hayo baada ya mkutano wake wa kila wiki huko Vatican. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema yanayoendelea Mashariki ya Kati ni zaidi ya vita na sasa ni ugaidi, bila kuweka wazi iwapo anauzungumzia uvamizi wa Hamas wa Oktoba 7 au operesheni ya kijeshi ya Israel huko Gaza.

Wiki iliyopita, Vatican ilisema inatarajia kwamba papa ataonyesha "ukaribu wake wa kiroho"katika mikutano hiyo ya faragha ambayo ilisema itakuwa ni mikutano yenye sura ya kiutu tu.

Soma pia:Israel na Hamas wafikia makubaliano ya kubadilishana mateka

Israel na Hamas leo wametangaza makubaliano ya kuwaachia huru mateka 50 wa Israel na wafungwa kadhaa wa Palestina walioko Israel na pia usitishwaji wa mapigano wa siku nne.