1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ataka vita visitishwe Gaza

Amina Mjahid
22 Oktoba 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, ametoa wito wa kumalizika kwa mgogoro kati ya wanamgambo wa Hamas na Israel, wakati kukiwa na hofu kwamba mgogoro huo huenda ukatanuka.

https://p.dw.com/p/4XsNa
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ametaka mashambulizi yasitishwe bainan ya Israel na Hamas.
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ametaka mashambulizi yasitishwe bainan ya Israel na Hamas.Picha: Gregorio Borgia/AP/picture alliance

Papa ametoa wito pia wa misaada zaidi ya kiutu kuruhusiwa kuingia katika Ukanda wa Gaza. 

Katika hotuba yake ya kila Jumapili katika uwanja wa St. Peters mjini Roma, Papa aliye na miaka 86 alisema vita huleta madhara makubwa huku akishinikiza maeneo husika kufunguliwa, ili misaada iwafikie walengwa na akisisitiza kuachiwa huru kwa watu walioshikiliwa mateka na Hamas. 

Soma zaidi: Guterres atoa rai ya kusitishwa mapigano kuruhusu misaada Ukanda wa Gaza

Kumekuwa na wasiwasi wa kutokea mgogoro wa kibinaadamu baada ya Israel kusitisha huduma ya maji umeme na chakula kuingia katika eneo hilo linalokumbwa na vita. 

Tangua kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7 watu zaidi ya 6,000 wameuwawa katika pande zote mbili zinazohasimiana.