1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Bibi Royal ameteuliwa kugombea urais Ufaransa

26 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpA

Ségoléne Royal aliekuwa waziri wa mazingira wa zamani wa Ufaransa,ameteuliwa rasmi na chama chake cha kisoshalisti PS,kugombea uchaguzi wa rais mwakani.Katika kikao cha Novemba 16,Bibi Royal mwenye umri wa miaka 53,tayari aliteuliwa na chama chake kugombea urais.Wajumbe 1,300 wa chama cha PS katika mkutano maalum mjini Paris sasa wamethibitisha rasmi matokeo hayo.Chama chake,mwakani kitapambana na chama tawala cha kihafidhina cha rais wa hivi sasa Jacques Chirac.