1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Kundi la nchi 6 kujadili mswada wa azimio kuhusu Iran

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmZ

Nchi tano zenye kura ya turufu katika Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani zinatazamia kukutana siku ya Jumanne katika mji mkuu wa Ufaransa,Paris.Wanachama hao wanataka kushauriana juu ya azimio la Umoja wa Mataifa kuhusika na mgogoro wa kinuklia wa Iran. Ujerumani,Ufaransa na Uingereza ziliwasilisha kwa Marekani,Urussi na China mswada wa azimio la Umoja wa Mataifa,ukiwepo uwezekano wa kuiwekea Iran vikwazo.Mswada wa kwanza wa nchi za Ulaya uliopendekeza kuweka vikwazo,ulikataliwa na Urussi na China.