PARIS : Mgomo wa treni waingia siku ya sita
19 Novemba 2007Matangazo
Abiria wa treni nchini Ufaransa leo wanakabiliwa tena na usumbufu kutokana na mgomo wa usafiri wa treni kuingia siku yake ya sita.
Vyama vya wafanyakazi vimekuwa na mgomo huo kupinga mpango wa mageuzi wa malipo ya uzeeni.
Mgomo mwengine tafauti unapangwa kufanyika hapo kesho na wafanyakazi wa serikali wakiwemo walimu na wafanyakazi wa hospitali wanaopinga kupunguzwa kwa wafanyakazi na mageuzi kwa idara za serikali.