1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Mgowa wa usafiri waingia siku ya pili

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1E

Mamilioni ya abiria wa treni nchini Ufaransa kwa mara nyengine inabidi watafute njia za kwenda kazini wakati mgomo wa usafiri wa umma ukiingia siku yake ya pili leo hii.

Rais Nicolas Sarkozy anatowa wito wa kiumalizika kwa haraka mgomo huo wa kazi wa kupinga mpango wake wa mageuzi ya malipo ya uzeeni.Msemaji wake amesema mgomo huo hauna budi kukomeshwa kwa maslahi ya abiria hivi sasa wakati ambapo kuna mazingira ya kuanza mazungumzo na vyama vya wafanyakazi juu ya mpango huo wa mageuzi.

Huduma za treni zimepunguwa kuwa theluthi moja ya zile za kawaida kutoka mgomo wa hapo jana na kuathiri takriban wafanyakazi 500,000 wa sekta ya umma.

Mjini Paris treni moja tu kati ya tano za reli ya chini ya ardhi inafanya kazi.