1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Mkutano kuhusu Darfur waanza

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoU

Mkutano wa kimataifa kuhusu mgogoro wa Darfur unatarajiwa kuanza mjini Paris nchini Ufaransa leo hii.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice, na mwenziwe wa Ufaransa Bernerd Kouchner pamoja na washiriki kutoka Umoja wa Ulaya na pia kutoka bara la Afrika.

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice.

Mazungumzo yao yalilenga zaidi hali ya nchini Lebanon., Afghanistan, Kosovo, Iran na jimbo la Darfur.

Kabla ya mkutano huo kuanza bibi Rice amewaambia waandishi wa habari kwamba jumuiya ya kimataifa haiajfanya lolote kuutatua mgogoro wa Darfur.