1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Msaidizi wa Kifaransa amelazwa hospitalini Chad

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJp

Mfaransa mmoja miongoni mwa sita waliozuiliwa jela nchini Chad,kuhusika na madai ya kuwateka watoto 103 waliosema kuwa ni yatima kutoka Darfur,amelazwa hospitali kwenye kituo cha kijeshi cha Ufaransa katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena.Msemaji wa kijeshi mjini Paris amethibitisha habari hiyo lakini hakueleza zaidi.

Wafaransa hao 6 wanakabiliwa na uwezekano wa kufungwa miaka 20 ikiwa watakutikana na hatia.Wao ni wafanyakazi wa shirika la Kifaransa linalotoa misaada ya kiutu „Zoe´s Ark“ na wanasema walitaka kuwaokoa watoto hao na kuwapeleka kuishi katika familia nchini Ufaransa.