1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Mwanasiasa atimuliwa na chama chake kwa kauli za kibaguzi nchini Ufaransa.

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXB

Chama cha upinzani, Socialist Party, nchini Ufaransa, kimemtimua mwanasiasa maarufu kwa kutamka kwa mara kadhaa kauli za kibaguzi.

George Freche, ambaye ni mkuu wa baraza la kusini anadaiwa amekuwa akilalamika kwamba wachezaji wengi wa timu ya taifa ya Ufaransa ya mpira wa miguu ni weusi.

Siku ya Ahamisi iliyoopita mwanasiasa huyo alitozwa faini ya Euro alfu kumi na tano kwa matamshi ya kuwatweza raia wa Algeria walioshirikiana na Ufaransa wakati wa vita vya ukombozi wa Algeria.

George Freche anamuunga mkono mgombea urais Bibi Segolene Royal lakini matamshi yake yamekuwa fedheha kwa chama hicho kiasi miezi mitatu kabla ya uchaguzi unaotarajiwa wa urais.